Tutapigaje hesabu ya kiwango cha ubadilishanaji wa pesa za kigeni kwa ajili ya madai yaliyoidhinishwa?

Kuna mambo kadha ya kutilia maanani wakati unapolinganisha viwango vya ubadilishanaji wa pesa, na njia kadha za kupiga hesabu yake. Hebu tutumie mfano:
  • Marko anatoka Uingereza. Alilipishwa €500 na kampuni yake ya ukodeshaji gari kwa ajili ya ajali iliyotendeka Ufaranza. Madai yake ya €500 yaliidhinishwa leo na RentalCover.com.
  • Marko atalipwa kwa Pauni za Uingereza GBP.
Timu ya Madai ya RentalCover.com hubadilisha sarafu zilizolipishwa (kwa Marko hii ni Euro) kwa sarafu za malipo (kwa Marko hii ni Pauni za Uingereza GBP) kulingana na viwango vya uhamishaji vinavyopaitikana kutoka kwa jukwaa kadha za huhamishaji pesa. Viko afadhali kwa 3-5% kuliko viwango vya mabenki na afadhali kwa 4-6% kuliko mawakala wa kubadilisha pesa.